Na Mapuli Misalaba Shinyanga
Wapangaji watatu wa nyumba ya mzee Mkama aliyefariki dunia, mtaa wa Mwinamila kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro unaowakabili kati yao na mtoto wa mwenye nyumba ili kulinda usalama wao.
Wapangaji hao ambao ni Hidaya Gimbi, Faustine Longino pamoja na Felista Charles wamesema nyumba waliyokuwa wamepanga kwa muda mrefu ametokea mmoja wa watoto wa mzee Mkama aitwaye Neema Mkama na kuezua mabati ya nyumba waliyokuwa wamepanga bila sababu za msingi na kwamba wapangaji hao wamesema hawadaiwi kodi ya nyumba.
Waandishi wetu wamefika kwenye tukio hilo na kuzungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Mwinamila Rukia Athuman ambaye ameeleza kuwa taarifa za tukio hilo amezipokea leo majira ya jioni baada ya wapangaji hao kuezuliwa Mabati takribani 10 kwenye sehemu ya vyumba vyao.
“Majira ya saa kumi na moja nilipigiwa simu na mjumbe kuwa baada ya wapangaji wameezuliwa mabati kwenye vyumba vyao lakini baada ya muda mfipi wakaja hao wapangaji wakanieleza nikawauliza shida ni nini wakasema hatujui ila mwenye nyumba ameleta fundi kuezua mabati kwenye sehemu yetu ila kwenye chumba chake maana tunaishi naye kwake hajaezua” . amesema Mwenyekiti Rukia