Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (kulia) akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Esaye Mwakifulefule (kushoto) mara baada ya shirika hilo kutangazwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha watoa huduma bora za Bima katika hafla ya kufunga rasmi maonesho ya 46 ya Biashara ya kimataifa ya Sabasaba leo Julai 13,2022 katika viwanja vya Mwalimu julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika hilo Esaye Mwakifulefule (aliyevaa suti) akiserebuka kwa furaha akiwa na watumishi wengine walipokuwa wakitoka katika ukumbi wa mikutano wa DOM ilipofanyika hafla ya kufunga Maonesho ya 46 ya Biashara ya kimataifa ya Sabasaba leo Julai 13,2022 Dar es Salaam.
Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limepata ushindi wa jumla katika kipengele cha watoa huduma za Bima katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofikia tamati leo julai 13,22022 na kufungwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizugumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kufunga maonesho hayo Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika hilo Esaye Mwakifulefule amesema kuwa ushindi huo ni muendelezo wa ushindi walioupata kwenye maonesho ya mwaka jana na kwamba mafanikio hayo ni kutokana na huduma Bora wanazozitoa kwa wananchi.
"Mafanikio haya ni juhudi za makusudi zinazofanywa na uongozi mzima unaoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shitika hili Dk Edmond Elio na utayari wa wafanyakazi kubadirika na kuingia katika soko la ushindani. Hata leo ukija katika Ofisi zetu huwezi hata kuamini kama Shirika hili linamilikiwa na Serikali kwa Asilimia 100 kwa sababu licha kumilikiwa na Serikali lakini 'Mindset' zetu ni kama Shirika la Sekta Binafsi"
"Huu ushindi sio wa kwanza, mwaka jana tulishinda na mwaka huu tena tumeshinda pia, tunaamini hata mwakani tutaendelea kushinda kwa mara ya tatu mfululizo "amesema Mwakifulefule.
Ameongeza kuwa anafahamu kuwa kuna ushindani mkubwa wa kibiashara kutokana na uwepo wa Taasisi nyingine za Binafsi Bima lakini kutokana na huduma Bora wanazozitoa sambamba na kulipa kwa wakati kumewafanya wananchi kuliamini Shirika hilo na kuona umuhimu wa kupata huduma zake.
"Katika biashara ya Bima jambo la kwanza ni kuaminika sokoni na uaminifu unakuja tu pale mteja anapohitaji kulipwa apate malipo yake kwa wakati sasa sisi hilo kwetu ni jambo la kwanza ndani ya siku saba za kazi kama Vielelezo zimekamilika mteja anakua amelipwa kwa wakati"
"Biashara ya Bima haitaki longolongo mtu kapata ajali amekuja ameleta taarifa zake kama taratibu zote zimekamilika ndani ya siku saba mteja anapata stahiki yake. Sisi tumenyooka hatuna kona kona wala hatuna shida ya ukwasi lakini pia tunawafikia wateja kwa wingi sana kupitia mbinu zetu mbalimbali za masoko" ameongeza.