Na Dotto Kwilasa, DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Benki ya NMB imetenga kiasi cha shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kutoa mikopo ya kusomesha Watanzania wenye akaunti kwenye Benki hiyo na wale wenye kipato.
Prof. Mkenda amesema hayo leo Julai, 12 2022 baada ya kutembelewa na Mtendaji huyo Mkuu wa Benki ya NMB ofisini kwake Jijini Dodoma na kueleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuwainua Vijana kielimu.
Amesema mara baada ya mazungumzo hayo utekelezaji wake utakwenda kwenye riba ya asilimia 9 na kwamba kilichobaki ni kuhakikisha wanaaingia kwenye kurasimisha makubaliano hayo pamoja na kuzungumza na wataalamu wa Wizara na Katibu mkuu ili kuweka utaratibu wa kiwezesha watanzania kufaidi mikopo hiyo.
"Tumefurahi kwamba leo tumekutana na mtendaji Mkuu wa NMB kuzungumza masuala ya elimu na kubwa tulilozingumza ni lile tulilozingumza kwenye bajeti yetu,kuhusu mikopo kwa wenye akaunti kwenye Benki hiyo na Wenye kipato,tunaamini kupitia mazungumzo haya wanafunzi wengi watanufaika kwa kuwa watasaidiwa kielimu,"amesema
Amebainisha kuwa mikopo hiyo itakuwa ya aina mbalimbali na kufafanua kuwa kwa wazazi wenye kipato cha juu ikiwa watataka kúwasomesha watoto, riba yao itakuwa asilimia 9 na kila watakapo punguza deni riba itatozwa kwa kiasi kilichobaki.
"Haya ni matumaini makubwa kwetu Kwa kuwa tunaamini mpango huu utawezesha watoto wengi kusoma Vyuo vya ufundi na Veta kwa sababu kuna wazazi ambao pamoja na kwamba wana kipato lakini hawawezi kulipa ada kwa mkupuo hivyo itawasaidia kumudu gharama,"amesema na kuongeza;
"Nashukuru ujio huu kwa kuwa Mkurugenzi amejiambia kuwa Wamekuja kumuunga mkono Rais Samia baada ya juhudi zake za kutoa elimu bila ada na wao walitenga fedha kwa ufadhili wa kidato cha tano na chuo kikuu ambako kwa ujumla walitakiwa watoe kwa wanafunzi 200 kwa mchanganuo wa wanafunzi 50 wa Vyuo vikuu na wanafunzi 150 kidato cha tano na cha sita,"amefafanua Waziri Mkenda
Kutokana na hayo amesema wamekubaliana kwamba tutakuwa na mfumo wa makubaliano kwa kuwa na wao kama Wizara kuputia bajeti ya Serikali wametenga fedha kwa wanafunzi waliofanya vizuri bila kujali kipato chao.
"Tukiunganisha nguvu ya Serikali,bodi ya mikopo na Benki ya NMB idadi ya wanafunzi watakaonufaika na masomo itakuwa kubwa,tutaendelea na mazungumzo kwa mwendo huu wa kutoa riba ya asilimia 9 kwa kusomesha watoto wetu,"amesema
Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana ya elimu nchini amesema pia ndani ya Wizara wanapokuwa na miradi fedha zote wataziweka kwenye Benki hiyo na kueleza kuwa hakuna sababu ya kupeleka sehemu nyingine ambazo hazitoi sapoti ya elimu.
"Natoa wito kwa Mabenki mengine kufuata nyayo za Benki hii ili kuwasaidia watoto na kurahisisha gharama za elimu kuwezesha kila mtoto kupata haki ya elimu bora,"amesema
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema Benki hiyo kwa kushirikiana na Wizara hiyo itaendelea kúwasomesha na kuwapa udhamini wa masomo ya nje ya nchi wanafunzi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa watoto kielimu.
Ametaja ajenda ya mazungumzo hayo kuwa ilikiwa ni mbili huku akiweka wazi kuwa ya kwanza ni ile ya bilioni 200 ambazo waliahidi toka mwanzo kwa watoto waliotakiwa kwenda kwenye masomo ya elimu ya juu na kukubaliana sasa watatoa riba kwa asilimia 9 badala ya 10.
"Nadhani hili ni jambo jema kwa wazazi wenye watoto walikosa mikopo ya Serikali na hivyo watapata kutoka kwetu ambapo tutasomesha vijana wenye mazingira magumu,wengine hawana wazazi na wengine Wana wazazi tutaangalia kigezo cha mazingira magumu,"amefafanua Mtendaji huyo wa NMB na kuongeza;
Huu ni mwanzo tu lakini tutaongeza zaidi idadi ya wanafunzi hapo baadae Kupitia wafadhili wetu na kwa kutumia washirika wa kimkakati Ili kuwanufaishà watoto wa kitanzania ,"amesisitiza
Social Plugin