PROF. MKENDA AANZA ZIARA YA SIKU SABA ROMBO


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda.

Na Mathias Canal, KILIMANJARO.


Mbunge wa Jimbo La Rombo ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameanza ziara ya kikazi ya siku saba Jimboni kwake Rombo Mkoani Kilimanjaro huku akiwataka Wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuboresha elimu.

Katika ziara hiyo,Mkenda amesema pia amekusudia kuwaeleza wananchi umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na juhudi zinazofanywa na serikali kupitia Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso za kumtua ndoo mama kichwani.

Akiwa ziarani katika kijiji cha Urauri Kata ya Reha, Wikayani Rombo Prof. Mkenda ameeleza dhamira ya kuwatumikia wananchi katika jimbo lake na umuhimu wa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.

Amesema kipindi cha nyuma kulikuwa na kampuni ya Kili Water iliyoanzishwa kama kampuni kutoa huduma ya maji Rombo lakini haikuwa na uwezo wa kutoa maji ya kutosha.

Amesema Wakati huo ilitolewa Bilioni 4 pekee na serikali kuimarisha upatikanaji wa maji jambo ambalo lililorudisha nyuma ulatikanaji maji hivyo kutofaa kwa mfumo huo ambapo kulipelekea kuiondoa kampuni hiyo ili kuimarisha upatikanaji wa maji.

Prof Mkenda amesema kuwa katika hatua za kuimarisha upatikanaji wa maji serikali iliamua kuanzisha Bodi ya Maji Rombo inayoitwa ROMBOWASA ambayo inawajibika kutengewa bajeti na serikali kwa ajili ya sekta ya maji.

Mbunge huyo amesema kufuatia kuanzishwa kwa ROMBOWASA, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 10 kwa wananchi wa Rombo kwa ajili ya upatikanaji wa maji ambapo hadi sasa wataalamu wanaangalia vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji yanafika kwa wananchi.

"Rais Samia amekuja kuwatumikia watanzania na tayari kwa sasa ameonyesha njia na ninawahakikishia wananchi tatizo la maji litakamilika ndani ya muda mfupi" amesema Prof Mkenda 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post