Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizugumza kwenye kikao cha Kikosi kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya elimu Duniani mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao. |
Na Mwandishi wetu, KILIMANJARO
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa imeamua kufanya mageuzi ya elimu na kwamba hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu rasimu ya Mitaala mipya pamoja na rasimu ya mapitio ya sera itakuwa imekamilika.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Julai 25,2022 wakati akizugumza kwenye katika kikao cha Kikosi kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya elimu Duniani mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Amesema Serikali ya Tanzania imejipanga vyema kuhakikisha elimu inaboreshwa na kufikia Mwezi Januari mwaka 2023 inatarajia kuanza mchakato wa kufanya maamuzi baada ya Rasimu hiyo kuwa imekamilika.
Pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Elimu wa Namibia Mhe Ester Anna Nghipondoka, Naibu waziri wa Elimu, Bosnia na Herzegavina Mr Adnan Husic, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Katibu wa Tume ya Kitaifa ya Elimu ya Qatar ya Utamaduni na Sayansi Mr Ali Al-Marafi.
Mchakato wa magezi ya elimu nchini Tanzania ulitokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili 2021 kuhusu mabadiliko ya Mitaala ya elimu na muelekeo mpya katika sekta ya elimu aitakayo.
Social Plugin