Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella akiongea wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sayansi, Uhandisi ,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Leo Julai 18, 2022 Jijini Arusha.
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa wiki ya Sayansi,Uhandisi ,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela Leo Julai 18,2022 Jijini Arusha.
Mhadhiri kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dkt. Emmanuel Mpolya akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sayansi , Uhandisi, Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela leo Julai 18,2022 jijini Arusha.
Washiriki wa ufunguzi waa Wiki ya Sayansi,Uhandisi,Teknoloji na Ubunifu ya Nelson Mandela wakifuatilia mada mbalimbali leo Julai 18,2022 Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na Waalimu kutoka shule za msingi Kikwe na Nambala mara baada ya ufunguzi wa Wiki ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia ya Nelson Mandela leo Julai 18,2022 Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Ndaki (Deans) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela mara baada ya ufunguzi wa Wiki ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia ya Nelson Mandela leo Julai 18, 2022 Jijini Arusha.
...............................................
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella ameipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia tafiti na bunifu zinazofanywa na Taasisi hiyo.
Mhe. Mongella ameyasema hayo leo Julai 18, 2022 jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa wiki ya Sayansi, Uhandisi ,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela ambayo huadhimishwa kila Julai 18 na kueleza kuwa tafiti na bunifu zinazofanywa na Taasisi hiyo zimesaidia kutatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
“Taasisi hii ni ya kipekee, tunajivunia na mchango wake tunaona kupitia tafiti na bunifu zinazofanywa na wanataaluma wake, kwa hakika zimesaidia kutoa majibu ya changamoto mbalimbali zinzoikabili jamii yetu ” amesema Mhe. Mongella
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo , Profesa Emmanuel Luoga amesema kuwa silaha kubwa itakayookoa Bara la Afrika ni elimu hivyo lazima rasilimali zilizopo zipate wataalamu wa kutosha katika kuinua uchumi kwa kufanya tafiti na bunifu zenye tija kwa maendeleo ya nchi za Afrika ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Amesema katika kuadhimisha wiki ya Sayansi, Uhandisi, teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela Taasisi itashirikiana na wadau mbalimbali wa serikali, sekta binafsi, Shule za msingi na Sekondari pamoja na jamii katika kuendelea kuboresha tafiti na bunifu.
Aidha, ametoa wito kwa wanafunzi wa shule za Sekondari kukitumia chuo hicho kwa ajili ya kufanya tafiti na mazoezi ya vitendo katika masuala ya sayansi na teknolojia ili kupata wataalam wengi zaidi watakaoinua sekta ya uchumi kwa kuja na bunifu zenye tija kwa manufaa ya jamii.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Nelson Mandela Dkt, Lilian Pasape ambaye ni Mhadhiri wa Chuo hicho amesema kuwa maadhimisho hayo yatahusisha matukio mbalimbali ikiwemo huduma kwa jamii kwa kutoa kadi za NHIF kwa ajili ya kufadhili matibabu kwa watoto wasiojiweza, kutembelea mahabusu ya watoto , kushirikiana na Shule zilizopo jirani na chuo ili wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wapate hamasa ya kujifunza masuala ya sayansi na Teknolojia.
Social Plugin