Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKINDA ASHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISUKUMA 'SANJO YA BUSIYA' KUHAMASISHA SENSA KISHAPU



Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda akishuhudia burudani wakati akizindua Rasmi Tamasha la Utamaduni Sanjo ya Busiya, Negezi wilayani Kishapu.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda, akipiga Ngoma kuzindua Rasmi Tamasha la Utamaduni Sanjo ya Busiya, Negezi wilayani Kishapu.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

KAMISAA wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda, ametembelea katika Tamasha la Utamaduni Sanjo ya Busiya katika kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Agosti 23 mwaka huu.

Makinda ameshiriki Tamasha hilo la Utamaduni leo Julai 5, 2022 akiwa ameambatana na viongozi wa Serikali na Chama, na kuwasihi wananchi wa wilaya hiyo ya Kishapu washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa na kutoa taarifa sahihi kwa makarani.

Amesema anawapongeza Machifu kwa kuandaa tamasha hilo la Utamaduni, ambalo hufanyika kila mwaka kuanzia Julai Mosi hadi 7 kwa kuenzi masuala ya utamaduni, na kuhamasishana kushiriki mambo mbalimbali ya kijamii na Kiserikali.

Makinda ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, amesema Sensa ya watu na Makazi ni muhimu sana kwa Taifa kimaendeleo, na kuwaomba Machifu kupitia Tamasha hilo la Utamadani, walitumia pia kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu zoezi la kuhesabiwa Sensa.

“Matamasha ya utamaduni ni mazuri sana, katika kuenzi mila, desturi na tamaduni zetu za kale, na furahi kuwa hapa ambapo nimeona mambo mbalimbali ya kimila zikiwamo burudani za ngoma na katika nyimbo zao ujumbe wake ulikuwa ni kuhamasisha Sensa,”amesema Makinda.

“Ndugu zangu suala la kuhesabiwa Sensa ni muhimu sana na linafaida kubwa kwetu katika kugawana keki ya Taifa iende kwa uwiano sawa,”ameongeza.

Aidha, amesema katika zoezi hilo la Sensa ni kuhesabiwa mara moja tu, na wale wenye wake kuanzia wawili na kuendelea (Ndoa za Mitala) siku hiyo ya Sensa watahesabiwa kule watakapokuwa wameamkia.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wafugaji wa mifugo kuwa siku ya Sensa watoe ushirikiano kwa Makarani kwa kutaja idadi kamili ya mifugo yao, ili Serikali itambue kuwa ina idadi kiasi gani ya mifugo hapa nchini, na kuwavirahisi kuwapelekea huduma mbalimbali yakiwamo Madawa na kujenga Majosho kulingana na idadi ya mifugo iliyopo sehemu husika.

Naye Chifu wa Busiya Edward Makwaia, amesema wamekuwa wakifanya Tamasha hilo la Utamaduni kila mwaka kwa madhumuni ya kusherehekea Baraka walizopata za mavuno, pamoja na kuhamasishana kushiriki shughuli mbalimbali za kiserikali.

Amesema Tamasha la Mwaka jana, walikuwa na ajenda ya kuhamasisha kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kuchukua tahadhari ikiwamo na kupata Chanjo, lakini mwaka huu wameangukia kwenye tukio kubwa la kitaifa la kuhesabiwa Sensa, na kuahidi kupitia Tamasha hilo watahamasisha wananchi kushiriki kuhesabiwa Sensa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amesema Tamasha hilo la Utamaduni limekuwa likiunganisha watu na kuwa kama ndugu, na Machifu wamekuwa wakishirikiana na Serikali kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Aidha, Tamasha hilo la Utamadani la Sanjo ya Busiya hufanyika kila Mwaka ambalo huanza Julai Mosi hadi siku ya Sabasaba.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda akitoa elimu ya Sensa kwenye Tamasha la Utamaduni Negezi-wilayani Kishapu.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda akitoa elimu ya Sensa kwenye Tamasha la Utamaduni Negezi-wilayani Kishapu.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda akitoa elimu ya Sensa kwenye Tamasha la Utamaduni Negezi-wilayani Kishapu.

Chifu wa Busiya Edward Makwaia akizungumza kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda, (kushoto) akiwa na Chifu wa Busiya Edward Makwaia kwenye Tamasha la Utamaduni Negezi-wilayani Kishapu.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda, (kushoto) akiwa na Chifu wa Busiya Edward Mkwaia akimuonyesha Historia picha zenye historia ya Chifu wa eneo hilo.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda, akipiga ngoma kuzindua Rasmi Tamasha hilo la Utamaduni Sanjo ya Busiya, Negezi-wilayani Kishapu.

Machifu kutoka maeneo mbalimbali wakiwa kwenye Tamasaha hilo la Utamaduni.

Viongozi wakiwa kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Wananachi wakiwa kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Wananachi wakiwa kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Wananachi wakiwa kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda akiangalia Burudani ya Ngoma kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Burudani za Ngoma zikiendelea.

Burudani za Ngoma zikiendelea.

Burudani za Ngoma zikiendelea.

Burudani za Ngoma zikiendelea.

Maonesho ya Utamaduni yakiendelea kwenye Tamasha hilo la Utamadani.

Maonesho ya Utamaduni yakiendelea kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Maonesho ya Utamaduni yakiendelea kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Muonekano wa Ikulu ya Chifu Makwaia.

Awali Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Anne Makinda akiwasili kwenye Tamasha hilo la Utamadani, Negezi-wilayani Kishapu kutoa elimu ya Sensa.

Picha za pamoja zikipigwa kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha za pamoja zikipigwa kwenye Tamasha hilo la Utamaduni.
Na Marco Maduhu, KISHAPU.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com