MSHASHU AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU ZOEZI LA SENSA

 

Katikati ni Mbuge wa viti maalum Mkoa wa Kagera Mh. Benadetha Mshashu akizungumza


Mwenyekiti wa Taasisi ya umoja wa Amani Mkoa wa Kagera Bw. Maafudhi Abdumarik Mwijage
Diwani wa kata ya Kashai Mh. Ramadhan Kambuga
Baadhi ya wànanchi waliohudhuria mkutano

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mbuge wa viti maalumu Mkoa wa Kagera Mh. Benadetha Kasabango Mshashu amewataka wananchi kujitokeza siku ya sensa kuhesabiwa ili kuleta maendeleo katika Mkoa.

Ameyasema hayo Julai 27,2022 katika mkutano wa hadhara wa kata ya Kashai uliofanyika katika mtaa wa Rwome na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, amesema kuwa watu watakaposhiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na makazi itasaidia Serikali kupata takwimu sahihi.

Ameongeza kuwa karani wa sensa afikapo atazungumza na mkuu wa kaya ambaye ndiye atatakiwa kutoa taarifa sahihi za watu wote watakao kuwa katika kaya yake hivyo mkuu huyo wa kaya asiogope kujibu maswali yote kwa kuhofia kuvujisha siri za kaya.

"Karani wa sensa atakuwa amekula kiapo kwahiyo mambo yote utakayomueleza itakuwa ni siri hawezi kuyatoa nje na utamtambua kwa kitambulisho, mavazi pamoja na kuambatana na kiongozi wa mtaa"amesema Mshashu.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kashai Mh. Ramadhan Kambuga amewataka wananchi wake wa kata ya Kashai kujitokeza kuhesabiwa ili kuipatia Serikali takwimu sahihi ambayo itaweza kuleta maendeleo kulingana na idadi ya watu.


Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya umoja wa Amani Mkoa wa Kagera Bw. Maafudhi Abdumarik Mwijage amemshukuru Diwani wa kata ya Kashai Mh. Ramadhan Kambuga kwa mkutano wake ambao ulikuwa ukiyasema yale mazuri yanayoendelea kufanyika katika Serikali ya awamu ya sita na kuwataka vijana wote kujitokeza siku ya sensa ili kuhesabiwa.

"Vijana wenzangu wote jitokezeni kuhesabiwa ili tuweze kuwekwa kwenye utaratibu mzuri wa Serikali kwa ajili ya maendeleo" amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post