Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao
Bahati Msengi ambaye ni mkufunzi wa sensa amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni, Kata ya Kanyenye mkoani Tabora.
Mkufunzi huyo ambaye pia alikuwa afisa elimu kata ya Milambo, wilayani Kaliua mkoani humo, alihudhuria mafunzo ya siku 21 yaliyomalizika juzi Jumanne na kufungwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, katika Chuo Cha Ualimu Tabora.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo ni kifo cha kawaida kama vifo vingine vinavyotokea hospitalini.
Via Mwananchi
Social Plugin