Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na wahudumu wa afya wa hospitali ya Wilaya ya Rombo-Huruma ambayo ipo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Moshi .
Baadhi ya wahudumu wa afya katika hospitali ya Rombo-Huru wakimsikiliza kwa makini |
Na Mathias Canal,KILIMANJARO
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda leo 20Julai,2022 amewatembelea na kuwasalimu wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Rombo-Huruma ambayo ipo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Moshi akiwa katika siku ya pili ya ziara yake jimboni hupa.
Prof Mkenda amesema kuwa serikali itaendelea kufuatilia upatikanaji wa majukumu yote ya msingi ikiwemo upatikanaji wa madaktari bingwa,upatikanaji wa kutosha wa vifaa tiba na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya.
Amesema kuwa huduma zinazotolewa na taasisi za dini ni wazi kuwa zinatolewa kwa lengo kuu la kuhudumia wananchi lakini sio kwa ajili ya faida kama ilivyo katika taasisi zingine.
Prof.Mkenda amesema ,"ndugu zangu watumishi na viongozi wa hospitali hii ya Huruma msiwe na wasiwasi juhudi za serikali zinaendelea ikiwemo kuhakikisha tunaleta huduma ya Bima ya Afya kwa wote" amesema
Pamoka na hayo amewapongeza madaktari, wauguzi na uongozi wa Hospitali hiyo kwa ujumla kwa kazi kubwa na nzuri wanayoendelea kuifanya kuhakikisha wanaokoa maisha ya wananchi hususani wakazi wa Rombo.
Kutokana na hayo ameahidi kufuatilia na kutatua changamoto ya upungufu wa watoa huduma ya afya katika hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ya kadhia ya barabara inayoenda hospitalini hapo.
Kuhusu changamoto ya maji, Mbunge huyo amesema kuwa changamoto hiyo itapatiwa ufumbuzi hivi karibuni kwani tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 10 kwa ajili ya miradi ya maji wilayani Rombo
Social Plugin