Sehemu ya vikosi vya ulinzi vikiwa katika ukakamavu tayari kabisa kudhihirisha utayari wa tukio la maadhimisho ya siku ya kumbukizi ya mashujaa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi Kuhusu maandalizi ya siku ya mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Julai 25,2022 Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza kwenye viwanja vya mashujaa jijini Dodoma |
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa leo Julai 23,2022 ametembelea viwanja vyaashujaa jijini hapa na kukagua maandalizi ya awali ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa huku akiweka wazi kuridhishwa na maandalizi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo vya Mashujaa, Waziri Majaliwa amesema mbali na maadhimisho ya Sherehe hiyo ya mashujaa kufanyika kitaifa Jijini Dodoma,kila Mkoa utafanya maadhimisho hayo kwenye sehemu za minara ya kumbukumbu.
"Maandalizi ya awali yapo vizuri Sana ,Kamati tendaji kupitia kurugenzi ya maandalizi imefanya kazi kubwa na ya kukubalika kwani tumeshuhudia vikosi vya ulinzi vipo katika ukakamavu wa hali ya juu,ni wazi kazi hii iko sawa,"amesema Waziri Majaliwa
Pamoja na hayo pia ametumia nafasi hiyo kuitaka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kuendelea kuhamasisha Wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo huku akiitaka Ofisi ya maadhimisho iliyopo chini ya Ofisi ya waziri Mkuu kuendelea na maboresho zaidi katika viwanja hivyo.
Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa
hapa nchini hufanyika Julai 25 ya kila mwaka ambapo maadhimisho hayo kitaifa kwa mwaka huu yanafanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kuenzi mchango wa mashujaa waliopigana vita kulinda maslahi ya watanzania.