Na Andrew Chatwanga - Songea
Wananchi wa Kijiji cha Nakawale kata ya Mhukuru wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma (Jimbo la Peramiho) wamemshuru Mbunge wao wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utawala bora kwa kutimiza ahadi ya kuwapatia umeme licha kijiji hicho kuwa mpakani mwa nchi jirani ya Msumbiji.
Wakiongea kwa Nyakati tofauti na Mwandishi wa habari hizi walisema walikata tamaa kwa vile Kijiji hicho kipo mbali na makao makuu ya wilaya na kipo mpakani wakitenganishwa na mto Ruvuma lakini sasa Umeme umewashwa rasmi na kuzinduliwa na Jenista Mhagama mbunge wao.
Akizindua umeme huo Mheshimiwa Jenista Mhagama,alimshukuru
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha ambazo zimesaidia
kufanikisha mradi na sasa alicho wahaidi wananchi wa Kijiji hicho na vijiji
vingine vinavyopitia mradi huo umeme umewaka na kuwataka wananchi kuendelea na
kazi zao za uzalishaji mali kupitia kilimo na yeye muda wote atakuwa nao
kuhakikisha wanapa maendeleo.
Mhe. Mhagama alisema umeme ni fursa ya maendeleo na
kubadilisha mitazamo ya wananchi na mpakani hapo wamejenga soko kubwa la
kimataifa la mazao ambayo sasa kwa kuwa na umeme itasaidia sasa kukamilika kwa
mradi wa maji ambao Shirika la Masista la Chipole wameanza kusambaza maji
kwenye maeneo yao.
Mhandisi Mkuu wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma Hamis Sosthenes
aliyesimamia mradi huo alisema jimbo la Peramiho lina jumla ya Vijiji 56 kati ya
hivyo vjiji 32 vimeshapatiwa umeme vimewashwa nab ado vijiji 24 ambavyo viko
kwenye mpango wa REA awamu ya tatu mkandarasi yuko kazini anaendea na wao
wanamsimamia vizuri ili akamalishe mradi kwa wakati.
Mhandisi Sosthenes alitambulisha huduma mpya ambayo sasa itawapunguzia adha wanachi ya kusafiri umbali mrefu ili kupata huduma ya kuunganishiwa umeme na sasa watatumia NIKONEKT ambayo wanaomba kuunganishiwa umeme kupitia simu ,kwa kutumia huduma hiyo umem unaunganishwa kwa siku nne tu .