Vijana wenye hasira nchini Ghana katika eneo la Suame, wamempiga makofi, kumtukana pamoja na kummwagia maji mbunge wao, Osei Kyei Mensah-Bonsu, kwa kile walichokieleza kwamba licha ya kuwawakilisha bungeni, lakini hatimizi ahadi zake za kurekebisha miundombinu ya barabara.
Osei Kyei Mensah-Bonsu ni mbunge wa chama cha New Patriotic Party (NPP), alikuwa katika eneo hilo kuzungumza na wananchi juu ya mahitaji yao ikiwa ni pamoja na miundombinu duni.
Mbunge huyo amesema kuwa hana wasiwasi kuhusu tukio hilo kwa sababu vijana wangefanya vivyo hivyo kwa afisa yeyote wa serikali, na sio yeye pekee.
Social Plugin