***************************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe .Mary Masanja (Mb) amewataka watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji katika Sekta ya Maliasili na Utalii kwa kuanzisha bustani za wanyamapori ili kusaidia ambao wanashindwa kufika katika maeneo ya hifadhi.
Ameyasema hayo alipotembelea bustani ya wanyamapori ijulikanayo kama Serval Wildlife inayopatikana Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.
Aidha amewatoa wasiwasi wananchi kupuuzia taarifa zinasombaa katika mitandao ya kijamii zinazoonyesha wanyama wakiwa wanacheza na kulishwa na binadamu wakifikiria kwamba ni wanyama wa hifadhini na badala yake wajue kwamba hao ni wanyama wa kufugwa.
“Ningependa nitoe ufafanuzi kwa wananchi wafahamu kwamba Serikali imekuwa ikihamasisha uanzishaji wa mashamba, ranchi na bustani za wanyamapori lengo ni kufanya uhifadhi ili kuwawezesha wananchi ambao hawana uwezo wa kufika kwenye maeneo ya hifadhi waweze kufika kwenye maeneo hayo kwa urahisi.” Mhe. Masanja amefafanua.
Amesema Serikali ipo makini na amempongeza mwekezaji wa Serval Wildlife kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuanzisha bustani ya wanyamapori.
“Hawa ni wanyama wa kufugwa ambao wamechukuliwa wakiwa wadogo wamekuzwa na kufundishwa namna ya kuishi na binadamu tofauti na wanyama waliopo hifadhini” Mhe. Masanja amesisitiza.
Social Plugin