WAZIRI MCHENGERWA AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA NA WIZARA ZAKE KUANDAA MATAMASHA YA UTAMADUNI


Waziri wa Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari akitoa ufafanuzi juu matukio ya siku 7 yatakayofanyika katika Tamasha la kwanza la Utamaduni Mwaka huu ambalo linafanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,

************************

Waziri wa Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe Mohamed Mchengerwa amewataka Viongozi kuanzia ngazi za Mikoa na Wilaya kuhakikisha nao wanaandaa Matamasha ya Utamaduni katika maeneo yao ili kusaidia kuenzi fikra za Waasisi wa Taifa .

Agizo hilo amelitoa leo Dar es salaam wakati akitoa ufafanuzi juu matukio ya siku 7 yatakayofanyika katika Tamasha la kwanza la Utamaduni Mwaka huu linalotarajiwa kufunguliwa hapo kesho na Waziri Mkuu Mhe Kasimu Majaliwa katika Uwanja wa Uhuru

Sambamba na hayo amesema hakuna Taifa lisilokuwa na Utamaduni hivyo vijana wenye vipaji wajitokeze kuonyesha vipaji vyao kwani Serikali umetenga fungu la kuwasaidia kuviendeleza licha ya kuwapatia tuzo mbalimbali.

Hata hivyo amesema siku ya Julai 4 mwaka huu wataofanya tukio la kipekee kuanzia Saa mbili asubuhi kutakuwa na maandamano ya Amani kutoka Temeke mwisho hadi Uwanja wa Uhuru na Mgeni rasmi katika matembezi hayo anatajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe Joachim Chisano.

"Tamasha hili ni la kihistoria kwani halitamuacha mtu nyuma kutakuwa na ngoma mbalimbali za asili,vikundi mbalimbali vya muziki ikiwemo Taraabu iliyochezwa hata kabla ya Uhuru na baada na uhuru hivyo ni burudani na vipaji vingi vitatambuliwa na fursa za ajira "alisema Mchengerwa

Aidha anapenda kuwaalika watu wote kuhudhuria kujifunza mengi kwani ifikapo julai 7 mwaka huu Rais naye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post