Na Mwandishi wetu,Dar Es Salaam
KATIKA Mikakati ya kuboresha ubora wa huduma za uzazi, mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya Afya iko mbioni kuanzisha Idara ya Huduma za Uzazi, Mama na Mtoto Wizarani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza kwenye Halfa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa jengo la huduma za Afya ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya CCBRT Jijin Dar Es Salaam.
"Sisi Sekta ya Afya sasa hivi tunajikita kwenye ubora wa huduma na sio bora huduma, tumejipanga kama Wizara na tumefurahi umetukubalia kuivunja Idara ya Tiba na sasa Kitengo cha Huduma za Uzazi mama na Mtoto kitakua ni Idara" amesema.
Waziri Ummy pia amemshuruku Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ruhusa ya kujengwa kwa Hospitali ya Taifa ya Mama na Mtoto ambapo Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya imetenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.