Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud S. Kigahe akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa mara baada ya kutembelea banda la WMA katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) wakipata picha ya pamoja kwenye banda lao katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
WAKALA wa Vipimo Tanzania (WMA) wamepanga kuingia katika kuhakiki vipimo kwenye tax kwa kufunga tax meter ambazo zitasaidia kufahamu mteja ametembea akiwa kwenye tax kwa umbali fulani na kuweza kulipa fedha halali ambayo inalingana na umbali ambao ametembea.
Ameyasema hayo leo Julai 03,2022 Afisa Vipimo Mkuu WMA, Bw.Gaspar Matiku katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Amesema wamepanga kuhakiki Tax Meters kwa kuzifunga kwenye tax ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kujua umbali na fedha ambayo inatakiwa kulipwa na mteja ambaye amepanda tax kwenda sehemu ambayo anahitaji.
"Biashara ya Tax imekuwa kubwa na inatumika, sasa badala ya mtu kutamkiwa kwamba unatoka hapa ninakwenda shehemu fulani, huyu anakumbia utanipa elfu 20 na mwingine anakuambia utanipa elfu 30 kwahiyo hakuna usawa kwenye hiyo ruti". Amesema
Aidha amesema wamepanga kuingia kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la muda wa maongezi ili mtu anapolipia muda wa maongezi kama umeongea dakika fulani iwe ya kweli pamoja na sehemu ya kujazia upepo kwenye magari ili kuondokana na udanganyifu.