Watu watatu wamefariki dunia baada ya lori kugonga basi la shule katika Soko la Ntharene huko Imenti Kusini, Kaunti ya Meru.
Ajali hiyo imetokea leo Ijumaa August 26, 2022 majira ya asubuhi ambapo Basi hilo lililokuwa likielekea eneo la Kanyakine lilikuwa likisafirisha wanafunzi kuwapeleka shuleni wakati lori lililokuwa likielekea Nkubu lilipoteza mwelekeo na kusababisha ajali hiyo.
Watu watatu ambao ni madereva wawili na mwanafunzi walikufa papo hapo huku Wanafunzi zaidi ya kumi wakijeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Consolata, Nkubu.
Aidha Miili ya madereva na mwanafunzi huyo ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo.
Social Plugin