Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI KAMPUNI YA ASFA HOSE SERVICE WALIVYOHAMASIKA KUSHIRIKI KIKAMILIFU SENSA YA WATU NA MAKAZI AGOSTI 23

Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Co. Ltd inaungana na Watanzania wote kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022.

Wafanyakazi wa Kampuni hiyo yenye makao makuu Mjini Kahama mkoani Shinyanga na matawi yake Tabora na Mwanza wamesema wapo tayari kuhesabiwa huku wakitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi wote kushiriki katika zoezi la Sensa kwa ajili ya maendeleo ya taifa.


“Sisi Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Co. Ltd tupo tayari Kuhesabiwa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya taifa.. Ewe Mwananchi jiandae kuhesabiwa!! Sisi tupo tayari kuhesabiwa!!”, amesema Meneja wa Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Co. Ltd, Gabriel Mathew.

Tazama Video




KUHUSU KAMPUNI YA ASFA HOSE SERVICE AND MAINTENANCE SUPPORT CO. LTD

Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Co. Ltd inajihusisha na kubana hose pipe,kuuza vipuli vya mitambo,mashine na magari,kuuza vifaa vya kujikinga na hatari kazini (PPE),kuuza Filters za aina zote,ufundi wa kutengeneza mitambo mikubwa migodini, Pampu aina zote na magari.


Kampuni hii pia inajihusisha na kuchomelea na kuunganisha mitambo na kuagiza magari mapya kutoka nje ya nchi, kukodisha mashine kama Crane, Fork lift, Excavator, Dozer, Grader na Rolla.


Pia wanajihusisha na utoaji elimu kwa wachimbaji wadogo na jamii kuhusu umuhimu wa kutumia vifaa vya kujikinga na hatari kazini (PPE), usalama kazini na utunzaji mazingira pamoja na masuala ya Burudani ikiwemo kuandaa Matamasha ya michezo na muziki.

Huduma zinazotolewa kwenye Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Co. Ltd ni pamoja na Line Boring, Civil Works, Machine Hire, Supply of PPE, Industrial Filters, Supply of Spare Parts, Welding and Fabrications, Hydraulic Hose Assembly and repair, Maintenance and service contracts.


Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Co. Ltd inapatikana maeneo ya Asilimia Mia karibu na Front Oil Kahama Mkoani Shinyanga.


Mawasiliano yao ni 0715859321 au 0755067193 au 0767566233 au 0744446970 au Email : info@asfahoseservice.com Website : www.asfahoseservice.com na kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Instagram, Youtube @asfahoseservice

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com