Polisi jijini Nairobi wanamsaka mfungwa mwenye umri wa miaka 19, ambaye alitoroka katika Kituo cha Polisi cha Viwandani.
Katika kisa hicho cha Jumatano, Julai 27, Erickson Khata aliomba ruhusa ya kuoga na afisa aliyekuwa kwenye zamu alimsindikiza kuchota maji na kuoga.
Hata hivyo, Khata alitumia fursa hiyo kutoroka baada ya afisa aliyekuwa amemsimamia kujinafasi ili kumpa faragha. DCI inasema kuwa mfungwa huyo alitoroka akiwa amevalia suruali ya ndani pekee yake, na kuacha nyuma nguo zake zote.
"Afisa huyo alishuku kuwa kila kitu kilikuwa si sawa baada ya mtungi wa maji ya kumwagika kusimama ghafla, na kufuatiwa na kimya cha kishindo. Alipokwenda kuangalia, alikumbana na beseni la maji yaliyopakwa nusu, kipande cha sabuni na nguo za mfungwa, bila mfungwa kuonekana,” wapelelezi walieleza.
Khata alikuwa amezuiliwa katika gereza la mgao wa ulinzi wa juu jijini Nairobi baada ya kulalamika kuwa yeye ni mtoto mdogo.
Ni hadi alipopelekwa katika Hospitali ya Mbagathi, mnamo Julai 26, ambapo vipimo vilifanywa na kuthibitishwa umri wake ulikuwa wa miaka 19.
Kesi hiyo ilitakiwa kutajwa mahakamani siku aliyotoweka bila kujulikana aliko.
Social Plugin