Kamba ya katani
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema kuwa Karani wa Sensa ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Buchenjegele wilayani Igunga, aliyejinyonga mkoani humo aliacha ujumbe ambao ulihusisha mgogoro wa kifamilia baina yake na mke wake.
Karani huyo aliyefahamika kwa jina la Edmund Zakayo, amejinyonga Agosti 22, 2022, majira ya saa 10:00 ndani kwake kwa kujitundika juu ya kenchi ya nyumba kwa kutumia kamba ya katani iliyosokotwa .
Katika eneo la tukio hilo jeshi la polisi lilikuta ujumbe ambao uliandikwa na marehemu ukihusisha mgogoro wa kifamilia baina yake na mke wake, hata hivyo pamoja na barua hiyo marehemu aliacha nyaraka zote ambazo alikabidhiwa kama karani kwa ajili ya zoezi la sensa ikiwemo kishikwambi.
Chanzo - EATV
Social Plugin