Awali Tanesco ilitangaza kuwa Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya Luku kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.
Mapema leo Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Cliff Maregeli alisema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku huku akiwataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa Luku katika kipindi kilichobainishwa.
"Wananchi wazingatie tu kununua umeme wa kutosha ili waepuke usumbufu unaoweza kujitokeza," alisisitiza Msemaji wa Tanesco, Martin Mwambene.
Social Plugin