PHD MEDIA LINK, TAPA KUENDESHA SEMINA KWA VIJANA WALIOHITIMU KIDATO CHA 4 & 6 WAKIJIANDAA KUJIUNGA CHUONI


Karibu ujisajili  kwa ajili ya mafunzo ofisi za PHD MEDIA LINK jengo la TEPU HOUSE Barabara ya Uganda mjini Bukoba-Maarufu kwa Mzee Ngeze.Simu 0767489094 

Email: phdmedialink@gmail.com

 KWA NINI KIJANA AANDALIWE  KISAIKOLOJIA KABLA YA KUJIUNGA CHUONI?

Ni kundi ambalo miezi michache  usoni linahama kutoka kwenye uangalizi wa karibu wa wazazi na walimu na kwenda kuanza maisha mapya vyuoni.

Wanakwenda kujitegemea kama watu wazima.Watakuwa huru kupanga vyumba mitaani.Watakuwa huru mchana na usiku.


Wengi wao ni vijana na mabinti wadogo ambao baadhi yao ni matunda ya sekondari za Kata.


Ni matunda mabichi ambayo ndoto zao lazima zilindwe.Wanakwenda kwenye dunia nyingine tofauti.Watasoma kozi moja na maofisa waliotokea kazini wanalipwa mshahara na kulipiwa ada.


Wapo mabinti waliosoma shule za bweni na walidhibitiwa kwa ulinzi mkali wa mageti,mbwa wakali na walinzi.Waliambiwa wanaume ni wabaya wakae mbali nao.


Sasa wanakwenda vyuoni.Wanatakiwa kusimama kwa miguu yao wenyewe.Sekondari waliambiwa wanaume ni wabaya ambapo katika hatua ya chuo watahitaji msaada wao.


Kule kila kitu kinakuwa kipya na hakuna anayeulizwa ulipata daraja la ngapi au ulikuwa wa ngapi Kitaifa.Kule wanasomea kazi.Ni wataalamu wajao wa nchi hii.


Ni vijana wadogo ambao kwa furaha wamenunuliwa simu.Haya ni sawa na mabomu yaliyofungwa shingoni mwao.


Kupitia simu hizo watapata marafiki wema na wabaya.Wataunganishwa na dunia hata kupata ahadi za kupelekwa Ulaya.


Watapenda kujaribu kila kitu.Watarekodi picha na mengine.Katika hatua hii kwa usalama wao ni lazima wafundishwe makali yaliyopo kwenye Sheria ya Mtandao.


Kwa kutojua makali ya sheria hiyo hata kabla ya kwenda vyuoni tayari wameanza kukosea.Kundi hili limeomba udahili na Mkopo wa masomo kupitia kwa watoa huduma za Intanet.


Kwa mara ya kwanza wengi wao wamefungua barua pepe(email) kama sehemu ya hitaji muhimu wakati wa maonbi.


Kwa bahati mbaya nywila(nenosiri)la barua pepe zao wameviacha kwa watoa huduma.Hawana udhibiti wa email zao.Zinaweza kutumiwa na mtu mwenye nia mbaya kufanya uhalifu kupitia mtandaoni.


Hiili ni kosa la uzembe wa kushindwa kudhibiti njia yako ya mawasiliano.Ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo.


Ili kuliandaa kundi hili na changamoto lukuki za maisha ya vyuoni PHD MEDIA LINK kushirikiana na CHAMA CHA WANASAIKOLOJIA TANZANIA(TAPA) watatoa mafunzo ya siku tatu mjini  BUKOBA kwa wahitimu wenye uhitaji


TAPA ni Chama cha kitaaluma miongoni mwao ni Wahadhiri wa somo la SAIIKOLOJIA vyuo vikuu na maeneo mengine 


Ni wabobezi wa kuhusu maisha ya vijana ambao ndoto zao ziliyeyuka baada ya kukosa msaada wa Kisaikolojia na wengine kujikuta wanachukua uamuzi usiofaa.


Suala la wanachuo kuishi kama "mme" na "mke" sio habari mpya ambapo suala hili lina uhusiano na masuala ya Kisaikolojia.Wataalamu wataendesha darasa litakalokuwa na mifano hai kwa vijana.


Kwa vyovyote vile kijana ambaye hakuwahi kumiliki 200,000,kesho apewe 3,000,000 kutoka Bodi ya Mikopo atafanya matumizi kwa fujo kwa kuwa hakuandaliwa.


Baada ya fedha kupukutika hawezi kumudu hata mlo mmoja.Ili kupunguza ukali wa maisha pengine hao ndiyo vijana wanaoishi"geto"na mabinti kudaiwa kuingia mitaani usiku.


Litakuwa darasa huru la kuwafungua vijana kuhusu ugumu wa safari inayokuja.Wanatakiwa kujengewa uwezo kuhusu maisha yao ndani na nje ya chuo.


Mabinti watajengewa uwezo wa kujiamini na njia za kuchukua uamuzi sahihi ili wafikie matarajio yao.Binti atafundishwa njia za kukwepa mitego ya kumpeleka kwenye anguko.Ataweza kuitikia miadi ya mwanaume yeyote kwa kuwa atakuwa anajua jambo la kufanya.Hawezi kusubiri usiku uingie ili aombe nauli.Atakuwa amejipangia muda na ukifika anaaga na kuondoka kwa kuwa amefanya maandalizi ya nauli.


Ni darasa la kufundisha na kuwaonya vijana kwamba wanaitwa watu wazima lakini bado ni wadogo wasijaribu kupima kina cha maji kwa mguu.


Bado wako kwenye rika la mcharuko na watapenda kujaribu kila kitu.Ni kizazi kinachopenda njia za mkato na mafanikio ya haraka.Vijana ambao hawakuandaliwa kuyajua haya mapema wametumbukia kwenye mitandao ya uhalifu na kuharibu kesho yao.


Wamejikuta mikononi mwa wauza unga.Wametelekezwa nchi za Mashariki ya mbali baada ya kuhaidiwa kazi nzuri.Wamejikuta kwenye madangulo.Sio kosa lao kwa kuwa hawakuandaliwa kabla KISAIKOLOJIA.


Wanatakiwa kujua kila kitu katika dunia ya utandawazi.Kwamba vyombo vya habari vinapodai kuna rushwa ya ngono vyuoni maana yake nini?Nani anatoa?Nani anapokea?Anapokelea wapi?Ukweli ni upi?


Yapo mengi ambayo ndani ya familia kijana hawezi kuyafahamu isipokuwa kupitia kwa wataalamu wanaotumia somo la SAIKOLOJIA kama Sayansi ya kukuza ustawi wa Binadamu.


Karibu ujisajili  kwa ajili ya mafunzo ofisi za PHD MEDIA LINK jengo la TEPU HOUSE Barabara ya Uganda mjini Bukoba-Maarufu kwa Mzee Ngeze.Simu 0767 48 90 94 email-phdmedialink@gmail.com



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post