Bei ya mafuta nchini Tanzania, imepanda tena mwezi huu na kuivuka ile ya Julai 2022 ambapo petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita na Sh179 kwa kila lita ya dizeli huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita kwa Jiji la Dar es Salaam.
Ewura imesema bei hizo mpya ambazo zitaanza kutumika Jumatano Agosti 3, 2022 zimejumuisha ruzuku ya Sh100 bilioni iliyotolewa na Serikali vinginevyo, lita ya petroli ingeuzwa Sh3,630 na dizeli Sh3,734 jijini Dar es Salaam.
Bei za Mafuta katika soko la dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia. Ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya bilioni 100 kwa ajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa Agosti 2022.