Cellie Mwambe kwenye picha akiwa na Baba yake
**
CELLIE Mwambe (14), ambaye ni mtoto wa Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe, amefariki dunia jana Agosti 23, 2022, baada ya kujirusha kwenye swimming pool ya nyumbani kwao maeneo ya Ada Estate Kinondoni Dar es Salaam, wakati akicheza na wenzake na kujigonga chini.
Akizungumza hii leo Agosti 24, 2022, kuhusu tukio hilo, mbunge huyo amesema kwamba, mtoto wake huyo baada ya kujirusha alienda upande wenye kina kidogo na kujigonga chini na kwamba alichelewa kutolewa majini ili kupelekwa hospitali.
“Hakukuwa na watu wazima karibu hivyo akanywa maji mpaka walipokuja kumuokoa ikawa ‘late’. Walivyomfikisha hospitalini ikashindikana kumuokoa, alifia hospitali baada ya kuwa amekunywa maji mengi nadhani hata pale alipojigonga alipata jeraha kubwa,” amesema Mbunge Mwambe.
Mwili wa marehemu Cellie unatarajiwa kuzikwa keshokutwa, Ijumaa, Agosti 26, 2022, jimboni Ndanda mkoani Mtwara.
Social Plugin