Aaron Matthew kijana mwenye umri wa miaka 19 aliyemuua Mama yake mzazi kwa kumchoma kisu zaidi ya mara 80
KIJANA mwenye umri wa miaka 19 Aaron Matthew raia wa nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha maisha Jela baada ya kukubali kuhusika katika mauaji ya mama yake mzazi ambaye alimuua kwa kumchoma visu zaidi ya mara 80 kisha kumkata sehemu ya koo.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alimuua Mama yake Ingrid Matthew mwenye umri wa miaka 54 kabla ya kumkata koo kasha kumtelekeza chumbani na kumuacha afariki.
Habari zinasema kuwa aliyefanikiwa kugundua mwili wake ni mumewe wa zamani ambaye alikuwa ameshatengana naye ambaye pia ni Baba wa Aaron Matthew aitwaye Andrew Marshall.
Aaron Matthew alijipeleka mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Cambridgeshire siku moja baada ya mwili wa marehemu kugundulika.
Aaron Matthew amemuua Mama yake mzazi kwa kumchoma kisu zaidi ya mara 80 pamoja na kumkata koo
Inspekta wa Upelelezi Nicole Main amenukuliwa akisema:
“Ni Aaron Matthew pekee ndiye anayeweza kuelezea ni kwanini aliamua kuchukua uamuzi wa kumuua mama yake mzazi.”
Natumaini hukumu hii itarudisha faraja kidogo kwa wote walioguswa na kifo cha mama huyu, ingawa kwa bahati mbaya hakuna hukumu ambayo inaweza kumrudisha duniani ingawa natoa salamu zangu za rambirambi kwa wote wakati wanaendelea na maombolezo ya msiba huu.
Social Plugin