Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame akitoa taarifa kwa wandishi wa Habari juu ya kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyekuwa amepanga kufanya mauaji ya mtu aliyekuwa akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mdogo.
Na Walter Mguluchuma - Malunde 1 blog Katavi
MTU mmoja aliyefahamika anayefahamika kwa majina ya Machia Mbasa (General) umri wa miaka 65 Mkazi wa Kijiji cha Lwafe Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kupanga njama za kutaka kumuua Mabula Ntemange(37) baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mdogo wakati yeye alipokuwa gerezani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa na jeshi la Polisi kufuAtia kupata taarifa za kutaka kufanya mauaji hayo yaliyotaka kusababishwa na wivu wa kimapenzi .
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo pia alimtuhumu Mabula Ntemange kuwa na mahusiano yake ya biashara alivyokuwa amejenga kijijini hapo na kuvitumia kwenye starehe na mke wake mdogo wakati yeye akiwa kwenye gereza la mahabusu la Mpanda kwa tuhuma za mauaji.
Baada ya jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kupata taarifa hizo waliweza kuchukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzima jaribio hilo kufuatia kuwa taarifa hizo kuwafikia kwa kuweza kumkamata mtuhumiwa Mbasa kabla hajatekeleza mauaji hayo.
Kamanda Ally Hamad Makame ameiambia malunde 1 blog kuwa baada ya mtuhumiwa kuwa amekamatwa alifikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajiri ya mahojioano zaidi juu ya kutaka kufanya kitendo hicho cha kutaka kukatisha uhai wa binadamu mwenzake .
Alisema baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alikiri kupanga njama za kutaka kufanya hivyo kutokana na hasira ya jirani yake huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake mdogo wakati yeye akiwa anasota mahabusu ambaye anadai kuwa anampenda sana.
Amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amewakodi wauaji wawili kutoka Kaliua Mkoani Tabora na baada ya wauaji hao kufika Mjini Mpanda walipokelewa na mtuhumiwa na kisha walihifadhiwa kwa ajiri ya kusubiri kutekeleza mauaji .
Mbali ya kupanga mauaji hayo mtuhumiwa Machia Mbasa amekuwa pia akituma ujumbe za vitisho vya mauaji kwa watu wawili ambao ni Charles Lugembe na Dogani Malima wote wakazi wa Kijiji cha Mwamkulu Manispaa ya Mpanda .
Mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa ili kuweza kubaini mtandao mzima anaoshirikiana nao kushiriki vitendo vya mauaji na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili