Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA YABEBA UBINGWA NGAO YA JAMII....MAYELE AWATETEMESHA SIMBA KWA MKAPA





MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara Timu ya Yanga imepindua meza baada ya kuongozwa bao mpaka kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani zao Simba mchezo wa Ngao ya Jamii ya kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu mechi iliyopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.



Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 15 likifungwa na Kiungo Mshambuliaji Pape Sakho akipokea pasi Clatous Chama hadi mapumziko Simba walienda wakiwa wako mbele ya bao moja.


Kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Bernard Morrison na Jesus Moloko mnamo dakika ya 49 Mshambuliaji hatari Fiston Mayele,aliisawazishia Yanga akipokea pasi ya Khalid Aucho


Mayele tena alirudi nyavuni mnamo dakika ya 80 baada ya kupokea pasi ya Dickson Job na kuwanyanyua mashabiki wa Yanga.


Kwa ushindi huo Mayele ameipatia taji la kwanza la Ngao ya Jamii msimu wa 2022/23 baada ya mwaka jana kufunga bao moja na kuipa taji tena.


Via Fullshangwe blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com