Kushoto ni Khamis Mgeja
Na Mwandishi wetu,Kahama
MWENYEKITI mstaafu wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) na mdau mkubwa wa michezo nchini pia mmoja wa wazee wa simba Mzee Khamis Mgeja alitumia siku ya Simba Day kumuomba mfadhili wa Timu ya Simba Mo-Dewj aangalie namna ya kusaidia uanzishaji wa Timu ya Simba katika Kijiji cha Kawe Kata ya Iyenze Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Mgeja ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa michezo akiwemo mjumbe wa mkutano mkuu CCM – Wilaya ya Kahama na mwandishi wa habari mwandamizi nchini Shija Felishian waliungana na wanakijiji kusherekea Simba day. Walioiandaa wanakijiji wenyewe.
Pamoja na sherehe ya Simba day pia ilifanyika kazi ya ufunguzi wa tawi la Simba ambapo Mgeni rasmi Mzee Mgeja alifungua tawi hilo na kutoa ujumbe mzito wa wadau wa michezo nchini.
Mgeja aliwapongeza wanakijiji kwa kuwa wana simba wengi zaidi kijijini hapo kwa kuwa mfano wadau kujikusanya na kuchangishana wenyewe na kupelekea kuchinja Ng’ombe kwa ajili ya simba day hili ni jambo halijawahi kutokea sehemu mbalimbali mijini na vijijini nchini mmeonesha kwa vitendo simba ni nguvu moja.
Mgeja amesema ushabiki hivi sasa na muitikio wa mapenzi ya michezo mbalimbali nchini umekuwa mkubwa sana na hasa kwa SIMBA NA YANGA.
Sasa hivi umepamba moto sana, aliwaomba wana simba mtambue kuwa sisi simba na yangu sio maadui kabisa ila ni watani wa jadi tu na mpira wa Tanzania huwezi kuuzungumzia pasipo Simba wala Yanga Tanzania wote tunajua na dunia inajua.
Mgeja alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wawezeshaji na wafadhili wa michezo Nchini kuanzia Mo, GSM, Azam Timu za majeshi JW,JKT,POLISI, MAGEREZA, KMKM, JKU pamoja na baadhi ya Halmashauri na majiji mfano:- Halmashauri ya Geita, Halmashauri ya Ruangwa, Manispaa ya kinondoni, Jiji la Dodoma na Jiji la Mbeya amepongeza kuwa mstari wa mbele kusaidia na kuendeleza michezo. Naomba wadau wengine waige mfano huo.
Mgeja pia aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira mazuri na rafiki ya kuinua michezo mbalimbali nchini na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wa michezo wachangamukie fursa hizo kwani michezo sasa hivi duniani ni uchumi na inatoa ajira kila mtu ni shuhuda wa hilo.
Katika tawi hilo la simba kawe walichagua viongozi ambao ni Pamoja na Philipo Nyeru mwenyekiti, Phabian Kuyera, Makamu mwenyekiti, Mandela Said Katibu wa tawi, Shija Paul Mhasibu, Said Ally Omary ,Mjumbe, Refansi Polepole Mjumbe Pamoja na Mzee Khamis Mgeja aliyepewa heshima ya kuwa mlezi wa tawi.
Social Plugin