Naibu waziri ofisi ya Mkuu kazi,Vijana, ajira na wenye ulemavu mhe. Patrobas Katambi, amesema hadi kufikia Agosti 14 mwaka huu Mwenge wa Uhuru tayari umeshatembelea jumla ya Halmashauri 135 kati ya 195 zilizopangwa kutembelewa.
Pia amesema umekagua, kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali 941 yenye thamani ya Sh bilioni 551.7 kati ya hiyo miradi 64 yenye thamani ya Sh. Milioni 847.6 ndiyo iliyobainika kuwa na dosari ikiwemo kukosa nyaraka na changamoto mbalimbali za kiufundi.
Katambi alitoa taarifa hiyo Wilayani Bahi eneo la Bahi Sokoni mkoani Dodoma wakati wa makabidjiano ya Mwenge Kati ya uongozi wa mkoa wa Dodoma na Mkoa wa Singida.
Alieleza miradi hiyo na Kwa Kasi na maelekezo ya wakimbiza Mwenge waendelee kuirekebisha ili kuwa Sawa Sawa, mwenge wa uhuru ni jicho la Rais, Samia Suluhu Hassan hivyo miradi itakapokuwa na dosari hawatasita kufichua.
Naibu Waziri huyo alisema, wakimbiza Mwenge huo wameweza kuhamasisha suala la lishe na kutoa elimu ya hamasa kwa wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi ikiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi, kwani Sensa ni Afya, ni barabara, zahanati Sensa ni maendeleo ndio uchumi, Sensa ni elimu, Sensa ni kila kitu hivyo ni muhimu Sana.
Akizungumzia fedha za mfuko wa maendeleo aliwapongeza wakimbiza Mwenge kwa kufanikiwa kukusanya fedha hizo zikizotolewa kwa ajili ya Mfuko wa vijana zaidi bilioni 847.6 na kuzirejesha serikalini.
Katambi amesisitiza kuwa Anaimani mikoa yote ikiwemo Dodoma watawasilisha Fedha hizo na kuhakikisha Fedha hizo zilizotolewa na Serikali zinarejeshwa Serikali kuu.
"Wewe fanya mchezo utakwenda na mwenge, usipotekeleza majukumu yako na kupunguza uzembe ubadhilifu "hivyo kila mmoja nasisitiza awe makini katika eneo lake.
Social Plugin