Mtoto aliyeshughudia tukio hilo akisimulia
Jovin Saimon (10) aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Uwanja iliyopo Halmashauri ya mji Geita amefariki baada ya kupigwa ngumi ya tumbo na jirani yake Haruna Amini (16) mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Mkombozi kwa kosa la Kushika Kanzu yake
Shuhuda wa tukio hilo anasema kipindi anampiga kosa lilikuwa ni kushika Kanzu yake ambapo alimvuta na kumpiga ngumi ya kwenye mbavu.
Baada ya tukio hilo mtoto huyo alilia na kwenda kumwambia mama yake kuwa ana maumivu kwenye ubavu ambapo mama yake alimwambia kuwa kesho yake ndiyo angempeleka hospitali.
Inaelezwa kuwa baada ya kufanya vipimo vyote waligundua kwamba bandama imejeruhika na damu inavujia ndani ya tumbo.
CHANZO - EATV
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Ally Kitumbu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mtuhumiwa bado anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi
Social Plugin