Mfano wa nguo za ndani
MWALIMU Mbunifu kutoka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA ) Chang'ombe, Dar es Salaam Emmanuel Bukuku akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la VETA kuhusu teknolojia ya kifaa cha kukaushia nguo za ndani kitakavyopunguza mangonjwa ya fangasi ya Ngozi na Ugonjwa wa Mfumo wa Mkojo (U.T.I ) katika kundi la wanawake na watoto, kwenye maonesho ya Kilimo na Ufugaji Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
*Kuwa suluhu ya kupunguza magonjwa ya ngozi na U.T.I
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia chuo cha Ufundi Stadi cha VETA Chang'ombe Dar es Salaam kimebuni kifaa cha kukaushia nguo za ndani kinachoitwa Dhydrator mashine lengo kupunguza, kutokomeza magonjwa yatokanayo na Fangasi ya ngozi pamoja na Ugonjwa wa Mfumo wa mkojo (U.T.I)
Pia Watanzania wametakiwa kukubali teknolojia ambazo zinabuniwa na wazawa ili kuwapa hamasa wabunifu katika kuendelea kuongeza juhudi za ubunifu ikiwa ni kuzinunua bidhaa.
Akizungimza kwenye Maonesho ya Kilimo na Ufugaji Kitaifa Nane Nane 2022 yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya Mbunifu wa Chuo hocho Mwalimu Emmanuel Bukuku amesema kuwa watanzania wanaamini bidhaa zinazotoka chini kuliko kuuamini zinazobuniwa na wazawa hivyo kunafanya ubunifu wa ndani usiendelee.
Mwalimu Bukuku amesema kuwa baada ya kuona changamoto ya uanikaji wa nguo za ndani aligundua kufanya ubunifu mashine ambayo itaondoa changamoto hiyo ya kukausha nguo hizo kwa muda mfupi na mashine hiyo inatumia umeme kidogo.
Bukuku amesema nguo za ndani mara nyingi zikifuliwa huwa zinaanikwa ndani hali inayowasababishia watumiaji kupata magonjwa kutokana na kukuza wadudu ambao wanasababisha magonjwa kama Fangasi.
Kilichomsababishia kubuni mashine hiyo Mwalimu huyo amesema kuwa aliona jamii ina changamoto ya kupata magonjwa kama vile Fangasi, ya ngozi na U.T.I kwa watu wazima na watoto hivyo kifaa hicho kitasaidia kupunguza magonjwa hayo au kuyatokomeza kabisha.
"Kwa upande wa afya hii ni teknolojia nzuri na jamii bado haijajua hii mashine kwa ubunifu huu tunaweza kuwakomboa watoto wengi wanaokumbana na magonjwa ya U.T.I na Fangasi, pamoja na wanawake hii inaweza kuwa mkombozi kwao."ameongeza.
"Katika maonesho ya mwaka huu ya Nane nane tumeweza kuja na teknolojia mpya ya kifaa, mashine ya kukaushia nguo za ndani," amesema Mwalimu Bukuku.
Bukuku amefafanua kuwa mashine hiyo ametengeneza kwa muda wa wiki tatu na kuifanyia majaribio ambapo ilionesha ipo vizuri na inauzwa kwa shilingi 350,000.
Amesema mashine ipo kama dressing table ambapo mtumiaji atanufanika na vitu viwili atatumia kukuangalia kupitia kioo na chini kukaushia nguo za ndani.
Social Plugin