Nyumbu
Wizara ya Maliasili kupitia Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere, imekabidhi Nyumbu zaidi ya 20 kwa wananchi jamii ya Wahadzabe eneo la Yaeda Chini wilayani Mbulu, ili kutekeleza ahadi ya kutoa nyama kwa jamii hiyo ili iweze kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa.
Akikabidhi Nyumbu hao kwa jamii hiyo RC Nyerere amewaomba wananchi hao kujitokeza na kutoa ushirikiano wa kutosha katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linaloendelea nchini.
Akipokea kwa niaba ya wananchi wa jamii ya Wahadzabe, kiongozi wa mila Athuman Magandula, ameishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi hiyo.
Zoezi la Sensa nchini litaendelea kwa siku saba.
Via >> EATV
Social Plugin