Mahakama ya Juu imeamuru tume ya uchaguzi IEBC kumpa mgombea urais wa Muungano wa Azimio Raila Odinga idhini ya kutazama sava za tume ya Uchaguzi katika Kituo cha Kitaifa cha Kujumlisha kura ambazo huenda zilitumika kuhifadhi na kusambaza taarifa za upigaji kura.
Mahakama pia iliagiza tume hiyo kumpa masanduku ya kura ya vituo mbalimbali vya kupigia kura kwa lengo la ukaguzi, ili kuchunguzwa na kuhesabiwa upya.
Vituo hivyo ni pamoja na Shule ya Msingi ya Nandi Hills na Sinendeti huko Nandi, Belgut, Kapsuser na Shule ya Msingi ya Chepkutum katika Kaunti ya Kericho; Vituo vya Kupigia Kura vya Jomvi, Mikindani na Wizara ya Maji katika Kaunti ya Mombasa; Shule za Msingi ya Mvita, na Majengo katika Kaunti ya Mombasa; Tinderet CONMO, katika Kaunti ya Nandi; Jarok, Gathanji na Shule ya Msingi ya Kiheo katika Kaunti ya Nyandarua.
Maagizo hayo yatamwezesha Bw Odinga na walalamishi wengine wa uchaguzi wa Rais kuthibitisha madai kwamba kura ziliibiwa.
Kulingana na agizo hilo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inahitajika kumpa Bw Odinga ufikiaji unaosimamiwa na seva zozote ambazo zinaweza kuhifadhi habari za kitaalamu zinazotumiwa kunasa nakala ya Fomu 34C ambayo ni jumla ya kura zilizopigwa.
Walalamishi wengine watakaopewa fursa ya kutazama sava hizo ni pamoja na mgombea mwenza wa Bw Odinga Martha Karua, Youth Advocacy for Africa (YAA), Peter Kirika, Khelef Khalifa, George Osewe, Ruth Mumbi na Grace Kamau.
IEBC pia iliamriwa kuwapa nakala za sera yake ya usalama ya mfumo wa teknolojia inayojumuisha sio tu sera ya neno la siri, matrix ya neno la siri na wamiliki wa nywila za usimamizi wa mfumo.
Pia watapewa Habari zozote kuhusu utumiaji wa mfumo huo wa teknolojiana viwango vyake vya kuutumia , mazungumzo yaliofanyika ndani yake kwa utambulisho , ujumlishaji wa kura, upperushaji matokeo na uchapishaji matokeo hayo.
Tukisalia katika masuala ya Teknolojia , IEBC itatoa sera yake ya usalama kuhusu utumiaji wa mfumo huo na idadi ya watu walioingia.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin