Enas Taleb
MWIGIZAJI mmoja wa Iraq amesema analishtaki Gazeti la Economist kwa kutumia picha yake kuelezea makala kuhusu wanawake wa Kiarabu kuwa “wanene” kuliko wanaume.
Enas Taleb alisema kuwa picha hiyo ilitumiwa nje ya muktadha bila idhini yake na ilikiuka faragha yake. Pia alidai kuwa ilikuwa ni picha iliyohaririwa.
Mwigizaji huyo maarufu na mtangazaji wa televisheni alisema katika mahojiano kwamba ameanza hatua za kisheria nchini Uingereza.
The Economist haikutoa majibu mapema kuhusu suala hilo baada ya kuulizwa maoni yake.
Enas Taleb amesema picha ilitumika bila idhini yake na ilihaririwa
Makala hiyo yenye kichwa ‘Kwanini wanawake ni wanene kuliko wanaume katika nchini za Kiarabu’, ilichapishwa mwishoni mwa mwezi Julai, kwa kutumia picha ya Taleb iliyopigwa miezi tisa iliyopita kwenye Tamasha la Kimataifa la Babeli nchini Iraq.
Makala hiyo ilielezeakuwa umaskini na vikwazo vya kijamii vya kuwaweka wanawake nyumbani ni miongoni mwa sababu kwa nini wanawake wengi wa Kiarabuni wazito kupita kiasi kuliko wanaume.
Taleb alitaja makala hiyo kuwa ni”tusi kwa mwanamke wa Kiarabu kwa ujumla na hasa wanawake wa Iraq”, akiuliza kwa nini Economist “inavutiwa na wanawake wanene katika ulimwengu wa Kiarabu na sio Ulaya au Marekani”
Akizungumza na televisheni ya al-Arabiyaalisema amekumbana na “maoni ya unyanyasaji” kwenye mitandao ya kijamii.
Pia aliliambia jarida la New Lines kuwa alikuwa na afya njema na mwenye furaha na jinsi anavyoonekana. “Kwangu hicho ndiyo muhimu,” alisema.
Social Plugin