Viongozi mbali mbali wa kimataifa wameendelea kutuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Kenya William Ruto kufuatia kutangazwa kwake Jumatatu kama mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 9 Agosti,2022.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema:’’ Ninawapongezaa Wakenya kwa uchaguzi wao mkuu wa amani na kutangazwa kwa Dr William Ruto kama Rais mteule. Tunatazamia kuendelea kufanya kazi na makaka na madada zetu nchini Kenya kuimarisha uhusiano wetu wa karibu. Tuko pamoja’’:
Katika ujumbe wake wa Twitter Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema ”Ningependa kumpongeza rais mteule wa Kenya William Ruto na watu wa Jamuhuri ya Kenya kwa kuendesha uchaguzi wa huru, haki na wa amani.”
Naye Rais wa Nigeria Mahammadu Buhari amesema "Ningependa kuwapongeza watu wa Kenya kwa uchaguzi wa amani, na matokeo yenye uwazi, ambayo kwa mara nyingine tena yanaonyesha kuwa mchakato wa demokrasia ,maadili na kanuni vinasalia kuwa njia bora kwa watu kwa kuwachagua viongozi wao na kuwawajibisha