Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akiwa katika hamasa ya kuhamasisha wananchi wa Mkoa huo kushiriki kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agosti 23 mwaka huu, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifuatiwa na msanii wa Singeli Msaga Sumu, na Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo, kushiriki kikamilifu siku ya kuhesabiwa Sensa na watu na makazi ambayo itafanyika Agosti 23 mwaka huu.
Amesema zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi ni la muhimu kwa kila Mtanzania,kwa sababu Serikali itapata idadi ya watu wake kamili na kuwa virahisi kutoa huduma kwao za maendeleo kwa uwiano sawa na kujitosheleza.
“Nawaomba wananchi wa Shinyanga mshiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Agost 23 mwaka huu, ili lifanikiwe na kuirahisishia Serikali kuwa na mipango mizuri ya maendeleo kwa wananchi wake na kuwapelekea huduma stahiki,”amesema Mjema.
Aidha, amewatoa wasiwasi wananchi kuwa zoezi hilo la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi hali husiani na tozo ya kodi ya kichwa, na kuwaonya watu ambao wamekuwa wakipotosha waache mara moja sababu hawana nia njema na Taifa kusonga mbele kimaendeleo.
Katika hatua nyingine Mjema, amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, kuwa siku ya Agost 14 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye Mbio za Shinyanga Madini Marathon na uzinduzi wa kipindi cha Thamani ya Madini, matukio ambayo yamelenga kuutangaza Mkoa huo wa Shinyanga.
Nao viongozi wa dini waliohudhuria kwenye hamasa hiyo ya Sensa, wamempongeza Mkuu wa Mkoa kwa ubunifu wake, na kuahidi kumuunga mkono kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kuhesabiwa Sensa kupitia madhabahu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.
Mkuu wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi.
Mbunge wa Vitimaalum Christina Mzava, akizungumza wakati wa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi.
Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, akizungumza kwenye hamasa hiyo ya kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi.
Askofu wa Kanisa la EAGT Raphael Machimu, akizungumza kwenye hamasa hiyo ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.
Viongozi wa kidini na kimila wakiwa kwenye Hamasa ya wananchi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hamasa ya kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia akizindua Medali, Jezi namba kwa ajili ya Mbio za Shinyanga Madini Marathon.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akiwa katika hamasa ya kuhamasisha wananchi wa Mkoa huo kushiriki kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agosti 23 mwaka huu, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifuatiwa na msanii wa Sengeli Msaga Sumu, Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga.
Burudani ikiendelea kwenye mkutano huo wa hamasa ya Sensa ya watu na makazi.