Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTANDAO WA TELEGRAM SALAMA ZAIDI KULIKO WHATSAPP KWENYE UDUKUZI


Na Mwandishi Wetu

Mtandao wa kijamii wa Telegram umeonekana kuwa salama zaidi kuliko mtandao wa WhatsApp ambao umejizolea umaarufu zaidi duniani.


Wataalamu wa masuala ya usalama wa kidijiti na mitandao ya jamii wamesema kuwa utafiti wao umeonesha kuwa mtandao wa Telegram unaweza kuhimili mashambulizi kutoka kwa wadukuzi kuliko mtandao wa WhatsApp.


Nchini Nigeria, moja ya nchi za Afrika zenye watumiaji wengi zaidi wa mitandao ya jamii, wananchi wengi wanahamia kwenye mtandao wa Telegram ili kukwepa kudukuliwa.


Waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakilalamika nchini Nigeria kuwa mawasiliano yao ya WhatsApp yanadukuliwa na kusababisha wanyanyaswe au kukamatwa na polisi.


Vitendo hivyo vya udukuzi vimepelekea wananchi wengi nchini humo waamue kuacha kutumia mtandao wa WhatsApp na kuhamia Telegram, ambayo ni salama zaidi.


Telegram, ambayo inazindua huduma mpya ya "premium" imepata watumiaji wapya zaidi ya milioni 700 kutoka sehemu mbalimbali duniani ndani ya mwaka mmoja tu, huku watumiaji wengi wakihamia mtandao huo baada ya kuvutiwa na umadhubuti wake wa kuzuia udukuaji wa taarifa zao za siri.


Maabara ya wananchi nchini Canada inayojulikana kama the Citizen Lab at the University of Toronto, imebaini kuwa vyombo vya dola nchini Nigeria vimekuwa vikitumia teknolojia ya kijasusi kutoka nchi ya Isreal kudukua taarifa za faragha za wananchi kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.


Wananchi ambao wamekuwa wakidukuliwa na vyombo vya dola kupitia WhatsApp ni pamoja na waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com