Hadi sasa bado mgombea Urais William Ruto, ameendelea kuongoza kwa asilimia 51.65, akifuatiwa na Raila Odinga mwenye asilimia 47.71.
– William Ruto (UDA) anaongoza kwa kura 1,377,854 (49.74%)
ZOEZI la kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu wa rais uliofanyika jana nchini Kenya, limeendelea usiku kucha wa kuamkia Jumatano huku Wakenya wakisubiri kwa hamu matokeo rasmi.
Ushindani mkubwa katika kinyang’anyiro cha urais ni baina ya wagombea wawili, naibu wa rais William Ruto na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga.
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC inakabiliwa na shinikizo la kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki. IEBC imekiri kwamba takribani vifaa 200 vya kielektroniki vya kuwatambua wapiga kura vilishindwa kufanya kazi kati ya vifaa 46,000.
Wananchi wengi wa Kenya wana matumaini na kura ya mwaka huu kuwa italeta mabadiliko katika maisha ya kila siku wakati wakikabiliwa na kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei.