Gari lililopata ajali
Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Iguguno Ushamba lililoko wilayani Mkalama mkoani Singida, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mwendokasi.
Taarifa hiyo imetolewa jana Agosti 10, 2022, na Kamanda wa Polisi mkoa Singida, Stella Mutabihirwa, na kusema kwamba dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha bila kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipohamia upande wa pili wa barabara na kupinduka mara tatu
Ajali hiyo imetokea kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam, Mwanza wakati abiria wa gari hilo wakitokea Arusha kuelekea jijini Mwanza ambapo watu watano kati yao walipoteza maisha papo hapo huku dereva wa gari hilo akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Singida.
Social Plugin