Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kwa Ufadhili wa International Media Support (IMS) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limehamasisha waandishi wa habari kuwa wanafika kwenye eneo la tukio ili kupata habari na taarifa za kutosha kuhusu kilichotokea.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kwa Ufadhili wa International Media Support (IMS) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
“Waandishi wa habari fikeni eneo la tukio, jitahidini kufika kwenye matukio ili mpate taarifa kwa kina kuhusu matukio",amesema Nyandahu.
Aidha amesema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari huku akiomba kuwe na mahusiano mazuri ya kiutendaji ili kuondoa migongano mbalimbali ili kuboresha mahusiano zaidi na kuimarisha ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari.
"Mnapoandika habari za masuala ya ukatili mzifanyie mwendelezo, mnapoandika habari zenu msiishie njiani andikeni matokeo ya kesi mahakamani ili jamii ijifunze na kuachana na matukio ya ukatili wa kijinsia", Afande Analyse Kaika kutoka Dawati la Jinsia.
Akiwasilisha mada kuhusu usalama wa waandishi wa habari, Mwandishi wa Habari Mkongwe, Paul Mabuga amesema mahusiano ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari yanategemeana hivyo ni vyema wakafanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SPC, Greyson Kakuru amesema waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wapo tayari kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi huku akiwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022.
Amesema wameendesha Mdahalo huo ambao ni wa pili, uliolenga kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kiutendaji kazi baina ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi, hasa wanapokutana kwenye matukio.
“Mdahalo huu ambao tunaufanya leo ni wa pili, ambapo awali tuliufanya AprilI 28 mwaka huu, na lengo kuu ni kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa majukumu,”amesema Kakuru.
“SPC kwa kushirikiana na UTPC na IMS tutaendelea kufanya mijadala ya namna hii mara kwa mara ili kuweza kutoa elimu zaidi kwa wanahabari na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia mradi wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari na kuimarisha mahusiano mazuri,”ameongeza.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog na Marco Maduhu
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru akisoma hotuba leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru akisoma hotuba leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).
Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga, Jeremiah Zitta akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC)
Mwandishi wa Habari Mkongwe, Paul Mabuga akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC)
Mwandishi wa Habari Mkongwe, Paul Mabuga akizungumza leo Alhamisi Agosti 4,2022 wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC)
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC)Ally Litwayi akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Mwandishi wa Habari/Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Estomine Henry akizungumza kwenye Mdahalo huo.
Picha ya pamoja wakati wa Mdahalo wa Awamu ya Pili wa Ulinzi na Usalama wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC).
Picha na Marco Maduhu na Kadama Malunde