Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MSANII MAARUFU WA VICHEKESHO ERICK 'HIVYO HIVYO' AFARIKI DUNIA


MSANII maarufu wa vichekesho, Zabogan Zabron (Sauti ya gharama) maarufu kama Erick ‘Hivyo hivyo’ amefariki dunia.

Taarifa zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa vichekesho, Tiny White, zinaeleza kuwa msanii huyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Tiny White amesema asubuhi ya leo alipigiwa simu na ndugu wa karibu wa Erick na kumpa taarifa za kifo chake.

Ameeleza kuwa Erick alikuwa mgonjwa ambapo hapo jana aliwasiliana naye na kumueleza kuwa alikuwa amevimba mwili mzima.

Erick amefariki dunia akiwa nyumbani kwa dada yake Kibaha mkoani Pwani.

Inaelezwa kuwa wiki tatu zilizopita mchekeshaji huyo alilazwa katika Hospitali ya Amana, Ilala Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com