Mahakama ya kinondoni imemhukumu Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makossa matatu.
Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.
Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mshtakiwa amekiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi kwa muda ili kumwandikia hukumu.
Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya amemhukumu mfanyabiashara huyo kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.
Mbali na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.
Awali, Wakili Makakala alidai kuwa mshtakwia anakabiliwa na kesi ya makosa ya Usalama barabara namba 284/2022.