Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Christina Mndeme (wa pili kulia) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma. (Picha na Fadhili Abdallah)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Christina Mndeme (wa pili kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Kilumbe Ng'enda (Kushoto0 akiwa katika kkutano wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Christina Mndeme (wa tatu kushoto) katika eneo la Bangwe manispaa ya Kigoma Ujiji.
(Picha na Fadhili Abdallah)
Wananchi wa Bangwe manispaa ya Kigoma Ujiji wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Christina Mndeme alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo hilo.
**
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka idara ya uhamiaji nchini na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoshughulikia watu wenye changamoto za uraia kulifanyia kazi jambo hilo kwa staha na kufuata taratibu za kisheria badala ya kutumia nguvu na manyanyaso.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Christina Mndeme akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Kigoma alisema kuwa chama hakikubaliani na matumizi ya nguvu mahali ambapo hakuna sababu ya nguvu kubwa kutumika na kusababisha malalamiko kwa wananchi.
Mndeme alikuwa akijibu malalamiko ya Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda ambaye alisema kuwa pamoja na mambo mengine kumekuwa na manyanyaso makubwa kwa wananchi kuhusu masuala ya uraia watu wakikamatwa na kuwekwa mahabusu, kuhojiwa kwa muda mrefu ikiwemo wengine kupigwa.
Mbunge huyo alisema kuwa matatizo ya uraia imekuwa chanzo kikubwa kwa wananchi wengi wa mkoa humo kushindwa kupata vitambulisho vya uraia (NIDA) ambapo licha ya watu wengi kuhojiwa mara nyingi lakini bado imediwa kuwa hawana sifa za kupata vitambulisho pamoja na kuonyesha nyaraka kuthibitisha uraia wao.
Ng’enda alisema kuwa matatizo hayo yameenda mbali zaidi kwa watuhumiwa wa masuala ya uraia kutolewa wilaya nyingine na kutakiwa kuripotiwa ofisi za uhamiaji Kigoma Mjini jambo ambalo limewafanya kutumia gharama kubwa wakati kila wilaya mkoani humo inazo ofisi za uhamiaji.
“Wananchi wamekuwa wakitumia gharama kubwa kushughulikia matatizo yao ya uraia na wanapohojiwa na kutaja kabila lao kuwa Wabembe hali inakuwa mbaya zaidi na kuonekana kuwa mamluki wasiostahili kuwepo nchini, jambo hili limeleta malalamiko makubwa kwa wananchi,”Alisema Mbunge huyo wa Kigoma Mjini.
Kutokana na malalamiko huyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,Christina Mndeme alisema kuwa lazima watendaji wa idara ya uhamiaji watumie weledi wa kazi badala ya kusukuma na dhana hasa kuhusu makabila kwani mikoa inayopakana na nchi jirani zimekuwa na muingiliano wa makabila.
Pamoja na maelekzo hayo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara amehimiza suala la watu kujitokeza kuhesabiwa katika sense ya watu na makazi August 23 mwaka huu na kutoa wito kwa wananchi kukataa na kuwafichua watu wenye nia mbaya ya kutaka kuvuruga zoezo hilo.