Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua, Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) ambapo Kabla ya uteuzi huo Hamissi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Rais Samia pia amemteua Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Kagaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbert Mrango ambaye amemaliza kipindi chake.
Social Plugin