Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATINGA NA TREKTA KURUDISHA FOMU UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

John Francis Haule akishuka kwenye Trekta wakati wa kurudisha Fomu Ubunge Afrika Mashariki Agosti 8,2022 jijini Dar es salaam
TAZAMA VIDEO HAPA

Wakati zoezi la kuchukua fomu za Ubunge wa Bunge la Afrika la Afrika (EALA) likielekea ukingoni  kijana John Francis Haule (37) amejitokeza katika kutia nia kupitia chama chake pendwa cha CCM.

Akizungumza wakati wa kurudisha fomu Haule amebainisha kuwa ametia nia hiyo kwa mujibu wa katiba ya nchi na mkataba wa Afrika Mashariki vikitoa fursa kwa wanachi wenye sifa  kuwania nafasi hizo za kuwa wawakilishi katika bunge la Afrika Mashariki.


John Haule ambaye ni mzaliwa wa Wilaya  ya  Ludewa mkoani Njombe, alitumia fursa hio kufafanua  mambo  kadha kupitia vyombo vya habari.

 

PONGEZI KWA MH RAIS SAMIA SULUH HASSAN

Akizungumza baada ya kurejesha fomu Haule alisema kuwa  Rais  Samia Suluhu Hassan  ambaye ni Mwenyekiti  wa CCM  ameboresha Demokrasia ndani ya  CCM na kwa nchi pamoja na kufungua diplomasia ya kikanda na kimataifa.

 

Akinukuu kitabu cha TANU NA RAIA  1962 kilichoandikwa na MWL. J.K.Nyerere  kuwa ‘Uongozi wa TANU unatokana na WATU na unapatikana kwa njia ya  HAKI’ kwa msingi huo Rais Samia ana uongozi shirikishi  usio na vitisho  wala lugha za kufedhehesha viongozi anao waongoza na wananch kwa ujumla wake, hivyo anaongoza kwa misingi ya Azimio la Arusha yaani kuzingatia utu,udugu na usawa. Kwa kuwa uongozi unapatikana kwa haki hivyo ni kwa manufaa ya watu ndio maana nasi tumejitokeza kuomba ridhaa pasipo mashaka wala woga kwakuwa uongozi wa Mhe. Samia ni wa diplomasia,sheria na demokrasia.

 

Hivyo ndiyo maana hata sisi wakulima tumekuja kutia nia tukiamini kuwa bado tunayo fursa ndani ya chama chetu Cha Mapinduzi nadhani mmeona  na usafiri wetu  wa trekta tukiienzi siku ya wakulima leo Nane Nane.

 

CHANGAMOTO ZA EALA NA EAC KWA UJUMLA

 Haule alisema mbali na azi kubwa iliyo  fanywa na mabunge yote ya EALA, ila kuna changamoto kubwa hususani wakati huu tukijiandaa na shirikisho la kisiasa yaani Political Federation  ama political Confederation( political union) hivyo muhimu sana kutatua hizi changamoto.

 

1.  Invisible parliamentary system (process and events)  yaani kutokuwa mubashara katika runinga za mataifa wana chama  imepelekea hili bunge kuwa kama mradi wa viongozi wa kisiasa kinyume na matakwa ya mkataba unavyoelekeza kuwa jumuiya ya Afrika Mashariki ni ya wananchi sasa inakuwaje wananchi wa mataifa haya wasipate fursa ya kuona bunge na shughuri zanazo endeshwa kawa kodi zao?

“Hivyo nikipata fursa nitawashawishi wa bunge sheria itungwe ili EALA ianze kuwa mubashara kwa runinga za mataifa yote. Mfano. Sheria iliyo ondoa mifuko na vifungashio vya plastiki ili tugwa EALA watu hawajui, sasa ni wakati muafaka wa kurekebisha hilo jambo. Pia hili limepelekea hili bunge na jumuiya kuwa na msisimko dhaifu wa kisiasa(weak political stimulus) kwa wananchi wa kawaida japo linafanya kazi kubwa yenye manufaa kwa wananchi wa mataifa haya yote”,alisema Haule

 

2. Impropotionate representation yaani uwakilishi usio kuwa na uhalisia kati ya idadi ya watu na wale wawakilishi wanao wakilisha huko EALA. Ni changamoto  kuwa na uwakilshi wa watu 9 wanaowakilisha  watu takribani Milioni 60 milioni kwa miaka 22 , sasa ifike kipindi lile bunge wawakilishi waongezwe  wawe angalau 20 toka katika  kila taifa  mwachama ili kutoa wigo mpana wa uwakilishi. Lakini pia wakati huu ajenda nzito zinaenda jadiliwa  mfano sheria za uundwaji wa shirikisho la kisiasa Political federation au political confederation hizi niajenda nzito zinazo hitaji watu wengi wenye mawazo  mseto ila ya kimajumui kama yale yaliyo andikwa katika   pepa iliyo wakilishwa na  Mhe. Rais Yoweri Museven wa Uganda kwenye chama chake cha NRM   ‘entitled towards closer cooperation  in Africa ( 1998”) hayo   yalijenga msingi wa uhuishwaji wa EAC 1999.


 Hivyo ni vyema kumpongeza Mzee Museven kwa maono yake makubwa akiwa mwana  majumui mwenzetu.Na kama  ingewezekana ningefurahi kuona Hongera hizi zina mfikia kupita ubalozi wa Uganda hapa Tanzania kuwa sisi vijana hususani wanamajumui tuna tambua mchango wake mkubwa kuelekea shirikisho la Afrika Mashariki yaani The East Africa Federation ama mtangamano wa Afrika Mashariki . Na hii ndio ilikuwa ndoto ya waasisi wa mataifa haya  akiwemo Baba wa taifa MWL. J.K. Nyerere aliyependekeza njia aliyoiita ’ bottom up approach’  kuelekea ONE AFRICA POLICY


3. Special EAC constituency in each member states  ( geo constituency) yaani kuwepo na majimbo mahususi ya kijiografia katika mataifa mwana chama  ( members states) ili kuhakikisha wabunge wote wanapo enda kuwakilisha EALA wana kuwa ni wa majimbo ili waweze kutoa mrejesho kwa wananchi kuhusu mwenendo na malengo pamoja na mstakabali mzima wa kuelekea   shirikisho. Pia hii itatoa fursa kwa wanachi kufahamu zaidi kuhusu jumuiya yao, maana wabunge watalazimika kupiga kampeni na kuchaguliwa na wananchi pasipo kupitia kwenye mihimili ya bunge, ya mataifa mwanachma. Pia hii itasaidia kuwaandaa wananchi kisaikolojia kuelekea kuwa na Dola moja la kisiasa yaani Political federation la sivyo hii jumuiya itabaki kuwa kama mradi wa viongozi waandamizi wa kiserikali tu hususani wa kisiasa, sasa ni wakati muafaka kuishusha jumuiya kwa wananchi ili wa shiriki kuchagua  wawakilishi wa EALA.pia kutaleta  systematic representation  maana huu uwakilishi wa sasa ni randomly ambao sio wenye afya kwa ukuaji wa jumuiya bali itabaki kueendeshwa kwa mlengo na matakwa ya viongozi walioko kwa wakati huo.

 

UJUMBE JUU YA KUTUMIA TREKTA WAKATI WA KUREJESHA FOMU

 

CCM kwa asili yake ni chama cha wakulima na wafanyakazi, hata Baba wa taifa Mwl J.K Nyerere 1995 akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma alisema  ‘ CCM ni chama cha wakulima na wafanyaKazi ambao wote ni watu maskini chama hiki hakijawa cha matajiri’

Hivyo mimi kuja kwa trekta ikiwa ni siku ya Nane Nane  ambayo ni sikukuu  ya wakulima  na wakilisha lile kundi la wakulima ambao ndio wanachama asilia wa CCM tangu TAA   ,TANU na ASP hatimaye CCM 1977.mpaka sasa  CCM haijaondoka kwenye asili yake  pamoja na falsafa zake za umoja,udugu pamoja na uzalendo.

Pia nimetumia treta ili kutoa hamasa kwa wazalendo wa Afrika hususani sie tunao unda jumuiya ya EAC kuwekeze zaidi katika kilimo maana uchumi wa mataifa haya unategemea kilimo kwa kiasi kikubwa. Pia ili kuweza kuishi ile dhana ya kujitegemea yaani self-reliant hasa katika chakula, pembejeo na dhana za kilimo kwa mtaifa haya yote.

Pia kilimo kitasaidia sana katika ukuaji wa biashara baina ya mataifa wanachama hii itapelekea  makusanyo ya kodi kuwa makubwa na kufanya  mfuko wa jumuiya ya EAC kuwa na fedha za kutosha ilikueendeleza malengo pamoja na madhumuni ya kuelekea shirikisho la Afrika Mashariki hatimaye badae kuifikia ile ndoto ya One Africa policy kama ilivyotabiriwa na viongozi wa OAU mwaka 1963 huko Ethiopia

WANAO MFAHAMU HAULE WA NENA

       Wakizungumza katika eneo la Lumumba CCM Jijini Dar es salaam  ndg  Emmanuel Mwasakanyama alisema kuwa anamfahamu Haule tangu akiwa tawi la CCM Tabata mapaka akiwa katibu wa CCM shirikisho  vyuo vikuu   UDSM. Alisema kuwa Haule ni kiongozi aliyehamasisha sana wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki katika shughuli za chama  2012 hadi 2014 akiwa chuo kikuu cha DSM.

 

Pia hata sasa kuna vijana wengi wako katika kazi za chama na wengine niviongozi wakubwa tu ndani ya serikali amabo walihamasika na kupewa kadi nae  wakati akiwa katibu wa CCM UDSM.

 Naye Seki Kasuga ambaye  aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa alisema kuwa anamfahamu Haule kama mtu mbunifu na mwenye bidii katika kazi zake hasa za kuhamasisha na kushawishi wale anao waongoza ili kufikia malengo. Nakumbuka mwaka 2013 nilishirikiana na Haule akiwa katibu CCM UDSM kuandaa kongamano la vijana vyuo vikuu lililoitwa  ‘Amsha amsha vijana vyuo vikuu lililofanyika katika ukumbi wa Meeda ulioko Sinza na mgeni Rasmi alikuwa Mhe. January Makamba’ hivyo i know the guy” aliongeza Seki.

Naye  Maria Kigalu aliyekuwa mlezi wa vijana UDSM katika tawi la Abiyani  alisema binafsi anamfahamu Haule ni kijana anayejituma sana katika majukumu yake.

 Kwa upande wake Prof. Mwaikambo  wa UDSM Udara ya uhandisi alisema kuwa kijana haule ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuibua mambo mapya na kuyasimamia hivyo kutia nia EALA ni moja kati ya juhudi nzuri kwa vijana.

 

Daudi Kayombo  Mwalimu wa shule ya Sekondari St Getrude Pwani aliye pata kusoma na Haule  katika shule ya Ludewa Sekondari alisema anamfahamu Haule kama mmoja kati ya waliokuwa washiriki wa zuri wa midahalo yaani  school debate akiwa shule.

 

Sambamba  naye  John Mushi  aliye kuwa naye UDSM(PSPA) aliongeza kuwa Haule alikuwa active sana katika class seminars kwa hiyo ni kumtakia tu kila la heri katika azma yake ya kutia nia kwenye Bunge la EALA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com