Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amewataka wana CCM mkoani Morogoro kuendeleza za umoja na mshikamano ili kukifanya Chama hicho kuwa imara.
Shaka ameyasema hayo leo Agosti 7, 2022 wakati akiwasalimia wanachama wa CCM waliokuwa wamekusanyika katika ofisi za makao makuu ya Chama hicho Mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya siku moja ya kutembelea Maonyesho ya Wakulima (Nanenane).
"Nafurahi kwa mapokezi haya makubwa, nashukuru kwa umoja na mshikamano. Endeleeni kushikamana, endeleeni kuwa wamoja," amesema Shaka na kuongeza ametembelea maonyesho ya Nanenane ambayo kwa Kanda ya Mashariki yanafanyika katika viwanja vya Nanenane mkoani Morogoro.
Social Plugin