MATOKEO YA MWISHO KURA YA URAIS UCHAGUZI KENYA KUTANGAZWA NA IEBC


Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati amewataka wananchi kutokuwa na hofu kutokana na kutofautiana kwa matokeo yanayotolewa na vyombo mbalimbali vya habari.

Alifafanua kuwa tofauti hiyo imeletwa na ukweli kwamba vyombo mbalimbali vya habari vinaingia kwenye tovuti kwa nyakati tofauti na kutumia mbinu zao katika kujumlisha matokeo.

Mwenyekiti wa tume hiyo alisema kuwa alikuwa na matumaini kwamba vyombo vya habari vingeungana na kuanzisha kituo kimoja cha kujumlisha matokeo ya kura lakini haijawa hivyo.

"Lakini nataka tu kuwafahamisha Wakenya kwamba tangazo la mwisho la matokeo ya urais litafanywa na msimamizi wa uchaguzi hapa Bomas. Tunatumai kufikia mwisho wa kujumlisha yatakuwa yamewiana na kufanana kwa sababu matokeo ni kutoka kwa chanzo kimoja. Kwa hivyo kusiwe na hofu kuhusu tofauti tunazoziona kwenye vyombo vya habari kwa sababu mbinu zao zinaweza zisiwe sawa."

“Mwisho wa siku matokeo yataainishwa kwa sababu yanatoka chanzo kimoja,” alisema.

Chebukati pia alitangaza kuwa maafisa wa kusimamia kura katika eneo maeneo bunge walikuwa wameanza kuwasili katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura.

Chanzo - BBC Swahili

 

Bofya ***HAPA*** KUONA LIVE MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU KENYA 2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post