Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Mh. Toba Nguvila akizungumza
**
Na Mbuke Shilagi Kagera.
Katibu tawala Mkoa wa Kagera Mh. Toba Nguvila amewataka viongozi wa dini pamoja na Baraza la Amani Mkoani Kagera kuuweka Mkoa huo madhabahuni na kuiombea jamii kuondokana na ibilisi anaye chafua Mkoa ambao kwa sasa umekithiri mauaji ya kujinyonga.
Akizungumza katika Ibada ya Kanisa la Kiinjili Tanzania KKKT Diyosis ya Kaskazini Magharibi Manispaa ya Bukoba amesema kuwa kwa sasa Ibilisi amekuja watu wamejisahau na kuchukua sheria mkononi na kuanza kuchinja watu kama ng'ombe na kusema kuwa jambo hilo halikubaliki.
"Tuna kazi ya msingi sana viongozi wa dini, viongozi wa Serikali tunayo Mabaraza ya Amani kwenye Mkoa, Wilaya na Kata lengo ni kuhakikisha kwamba jamii inakuwa na mtengo mzuri na utulivu sana",amesema Nguvila.
Social Plugin