Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi ameambata na wataalam wa Wizara ya Maji, RUWASA, Wizara ya Fedha na Mipango, OR-TAMISEMI na Benki ya Dunia nchini Afrika ya Kusini ili kujifunza namna nchi hiyo inavyoendesha miradi ya maji kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Pia Msafara huo wa Naibu Waziri unatembelea viwanda mbalimbali vinavyozalisha vifaa kwa ajili ya miradi ya maji.
Keshokutwa msafara wa Naibu Waziri utaelekea Harare nchini Zimbabwe kwa lengo hilohilo la kujifunza zaidi.
Wizara ya Maji kupitia RUWASA wapo katika utekelezaji wa matumizi ya dira za maji ya malipo kabla ya matumizi sambamba na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye uendeshaji wa skimu za maji vijijini.
Social Plugin